Episodios

  • Dibaji
    Oct 6 2025

    Inatupasa kuzaliwa mara ya pili kwa maji na Roho

    Mungu(God), hapo mwanzo alipoumba mbingu na nchi, Yeye pia aliumba ulimwengu wa milele, mbingu na jehanamu. Yeye pia aliumba mwanadamu kwa mfano Wake Mwenyewe. Hata hivyo, kwa kuwa mwanadamu wa kwanza, Adamu, alitenda dhambi mbele za Mungu(God), watu wote imewapasa kufa mara moja. “Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu” (Waebrania 9:27).
    Kifo cha miili yetu ndiyo njia ya kupita kwenda kwenye uzima wa milele. Wale wasio na dhambi wataingia katika ulimwengu wa milele wa mbingu na kufurahia milele furaha ya kuwa mtoto wa Mungu(God), ilhali wenye dhambi watatupwa katika “ziwa la moto na kiberiti” (Ufunuo 20:10) na watateswa mchana na usiku milele na milele.

    https://www.bjnewlife.org/
    https://youtube.com/@TheNewLifeMission
    https://www.facebook.com/shin.john.35

    Más Menos
    16 m
  • 1. Lazima Kwanza Tujue Dhambi Zetu ili Tukombolewe (Marko 7:8-9, Marko 7:20-23)
    Oct 6 2025

    Kwanza, ningependa kufafanua dhambi ni nini. Kuna dhambi zilizofafanuliwa na Mungu(God), na kuna dhambi zilizofafanuliwa na wanadamu. Neno dhambi, kwa Kigiriki, lina maana ya ‘kukosa shabaha.’ Linamaanisha kutopata sawa. Ni dhambi tusipoyafuata amri za Mungu(God) kwa usahihi. Hebu kwanza tuangalie dhambi kama zilivyofafanuliwa na wanadamu.

    https://www.bjnewlife.org/
    https://youtube.com/@TheNewLifeMission
    https://www.facebook.com/shin.john.35

    Más Menos
    30 m
  • 2. Binadamu huzaliwa wakiwa wenye dhambi (Marko 7:20-23)
    Oct 6 2025

    Kabla sijaendelea, ningependa kukuuliza swali. Unajifikiriaje wewe mwenyewe? Je, unadhani wewe ni mzuri kiasi au mbaya kiasi? Unafikiri nini?
    Watu wote wanaishi chini ya udanganyifu wao wenyewe. Huenda wewe si mbaya sana kama unavyofikiri, wala si mzuri sana kama unavyofikiri.
    Basi, unadhani ni nani ataishi maisha bora ya imani? Je, ni wale wanaojiona kuwa wazuri, au wale wanaojiona kuwa wabaya?
    Ni wale wa pili. Kwa hiyo, ni nani aliye na uwezekano mkubwa zaidi wa kukombolewa: waliotenda dhambi nyingi au waliotenda dhambi chache tu? Wenye dhambi nyingi wana uwezekano mkubwa zaidi wa kukombolewa, kwa sababu wanajijua kuwa wenye dhambi. Wanaweza kukubali vyema zaidi ukombozi ambao Yesu aliwaandalia.

    https://www.bjnewlife.org/
    https://youtube.com/@TheNewLifeMission
    https://www.facebook.com/shin.john.35

    Más Menos
    21 m
  • 3. Tukifanya mambo kwa mujibu wa Torati, je, inaweza kutuokoa? (Luka 10:25-30)
    Oct 6 2025

    Luka 10:28, “Fanya hivyo nawe utaishi.”
    Watu wanaishi wakiwa na udanganyifu mwingi. Inaonekana kwamba ni dhaifu hasa katika jambo hili. Wanaonekana kuwa werevu lakini hudanganywa kirahisi na hubaki wasiotambua upande wao wa uovu. Tumezaliwa bila kujijua, lakini bado tunaishi kana kwamba tunajijua. Kwa sababu watu hawajijui, Biblia hutuambia kwamba sisi ni wenye dhambi.
    Watu huzungumza juu ya kuwapo kwa dhambi zao wenyewe. Nao hawawezi kutenda mema, lakini hujipendelea kujieleza kuwa wema. Wanataka kujisifu kwa matendo yao mema na kujionyesha. Husema kwamba wao ni wenye dhambi, lakini hutenda kana kwamba ni wema sana.

    https://www.bjnewlife.org/
    https://youtube.com/@TheNewLifeMission
    https://www.facebook.com/shin.john.35

    Más Menos
    41 m
  • 4. Ukombozi wa Milele (Yohana 8:1-12)
    Oct 6 2025

    Yesu alitupatia ukombozi wa milele. Hakuna mtu katika dunia hii ambaye hawezi kukombolewa ikiwa anamuamini Yesu kama Mkombozi wake. Yesu alitukomboa sisi sote. Ikiwa kuna mwenye dhambi anayehangaika kutokana na dhambi zake, ni kwa sababu hajaelewa jinsi Yesu alivyowatoa kutoka kwa dhambi zote kwa kupitia ubatizo Wake.
    Sote tunapaswa kufahamu na kuamini siri ya wokovu. Yesu alichukua dhambi zetu zote kwa ubatizo Wake na amebeba hukumu kwa dhambi zetu kwa kufa msalabani.
    Unapaswa kuamini wokovu wa maji na wa Roho; ukombozi wa milele kutoka kwa dhambi zote. Unapaswa kuamini upendo Wake mkubwa ambao tayari umekufanya kuwa mtu mwenye haki. Amini kile alichofanya kwa ajili ya wokovu wako katika Mto Yordani na msalabani.

    https://www.bjnewlife.org/
    https://youtube.com/@TheNewLifeMission
    https://www.facebook.com/shin.john.35

    Más Menos
    1 h
  • 5. Ubatizo wa Yesu na Upatanisho wa Dhambi (Mathayo 3:13-17)
    Oct 6 2025

    Bwana Mungu(God) wetu amekata pingu za dhambi kwa ajili ya watu wote. Wote wanaotaabika chini ya dhambi ni watumwa. Yeye ameondoa dhambi zetu zote. Je, yupo yeyote ambaye bado anateseka kutokana na dhambi?
    Inatupasa kuelewa kwamba vita vyetu dhidi ya dhambi vimekwisha. Hatutateseka tena kamwe kutokana na dhambi. Utumwa wetu wa dhambi ulikoma Yesu alipotukomboa; dhambi zote zilikoma hapo hapo. Dhambi zetu zote zimefanyiwa upatanisho na Mwana Wake. Mungu(God) alilipia dhambi zetu zote kupitia Yesu, ambaye alituweka huru, milele.
    Je, unajua jinsi watu wanavyoteseka kutokana na dhambi zao? Ilianza tangu wakati wa Adamu na Hawa. Wanadamu wanateseka kutokana na dhambi walizorithi kutoka kwa Adamu.

    https://www.bjnewlife.org/
    https://youtube.com/@TheNewLifeMission
    https://www.facebook.com/shin.john.35

    Más Menos
    1 h y 39 m
  • 6. Yesu Kristo Alikuja kwa maji, kwa damu, na kwa Roho (1 Yohana 5:1-12)
    Oct 6 2025

    Je, Yesu alikuja kwa maji? Ndiyo, alikuja. Alikuja kwa ubatizo Wake. Maji ni ubatizo wa Yesu uliotolewa na Yohana Mbatizaji katika Mto Yordani. Ulikuwa ubatizo wa ukombozi ambao kupitia huo aliondoa dhambi zote za ulimwengu.
    Je, Yesu alikuja kwa damu? Ndiyo, alikuja. Alikuja katika mwili wa mwanadamu na akabatizwa ili kuondoa dhambi zote za ulimwengu, kisha akalipa mshahara wa dhambi kwa kumwaga damu juu ya msalaba. Yesu alikuja kwa damu.
    Je, Yesu alikuja kwa Roho? Ndiyo, alikuja. Yesu alikuwa Mungu(God), lakini Yeye alikuja kama Roho katika mwili ili kuwa Mwokozi wa wenye dhambi.

    https://www.bjnewlife.org/
    https://youtube.com/@TheNewLifeMission
    https://www.facebook.com/shin.john.35

    Más Menos
    1 h y 5 m
  • 7. Ubatizo wa Yesu ni Uhalisia wa Wokovu kwa Wenye Dhambi (1 Petro­3:20-22)
    Oct 6 2025

    Tulizaliwa duniani humu, lakini kabla ya hapo Mungu(God) alikuwa tayari anatujua. Alijua kwamba tungezalika tukiwa wenye dhambi na akatuokoa sisi sote waumini kupitia ubatizo Wake, ulioondoa dhambi zote za ulimwengu. Aliwaokoa waumini wote na kuwafanya wote kuwa watu Wake.
    Haya yote ni matokeo ya neema ya Mungu(God). Kama isemavyo katika Zaburi 8:4, “Mtu ni nani hata Umkumbuke.” Wale waliookolewa kutoka kwa dhambi zote ndio wapokeaji wa upendo Wake wa kipekee. Wao ni watoto Wake.

    https://www.bjnewlife.org/
    https://youtube.com/@TheNewLifeMission
    https://www.facebook.com/shin.john.35

    Más Menos
    33 m