JE, UMEZALIWA UPYA KWELI KWA MAJI NA KWA ROHO? [Toleo Jipya Lililorekebishwa] Podcast Por The New Life Mission arte de portada

JE, UMEZALIWA UPYA KWELI KWA MAJI NA KWA ROHO? [Toleo Jipya Lililorekebishwa]

JE, UMEZALIWA UPYA KWELI KWA MAJI NA KWA ROHO? [Toleo Jipya Lililorekebishwa]

De: The New Life Mission
Escúchala gratis

Obtén 3 meses por US$0.99 al mes

Somo kuu la kichwa hiki ni "kuzaliwa mara ya pili kwa Maji na Roho." Kina upekee kwenye mada hii. Kwa maneno mengine, kitabu hiki kinaeleza waziwazi maana ya kuzaliwa mara ya pili na jinsi ya kuzaliwa mara ya pili kwa maji na Roho kwa mujibu wa Biblia. Maji yanaashiria ubatizo wa Yesu katika Mto Yordani na Biblia inaeleza kuwa dhambi zetu zote zilipitishwa kwenda kwa Yesu wakati alipobatizwa na Yohana Mbatizaji. Yohana Mbatizaji alikuwa mwakilishi wa wanadamu wote na mzao wa Haruni, Kuhani Mkuu. Haruni aliweka mikono yake juu ya kichwa cha mbuzi wa Azazeli na kupitisha dhambi zote za mwaka za Waisraeli kwake katika Siku ya Upatanisho. Hii ilikuwa kivuli cha mambo mema yajayo. Ubatizo wa Yesu ni mfano wa kuweka mikono. Yesu alibatizwa kwa njia ya kuwekwa mikono katika Yordani. Hivyo Yesu alizichukulia mbali dhambi zote za ulimwengu kupitia ubatizo Wake na akasulubiwa ili kulipa kwa ajili ya dhambi hizo. Lakini Wakristo wengi hawajui ni kwa nini Yesu alibatizwa na Yohana Mbatizaji katika Mto Yordani. Ubatizo wa Yesu ndio neno kuu la kitabu hiki na sehemu muhimu sana ya Injili ya Maji na Roho. Tunaweza kuzaliwa mara ya pili kwa kuamini tu ubatizo wa Yesu na Msalaba Wake.© 2004 by Hephzibah Publishing House Cristianismo Espiritualidad Ministerio y Evangelismo
Episodios
  • Dibaji
    Oct 6 2025

    Inatupasa kuzaliwa mara ya pili kwa maji na Roho

    Mungu(God), hapo mwanzo alipoumba mbingu na nchi, Yeye pia aliumba ulimwengu wa milele, mbingu na jehanamu. Yeye pia aliumba mwanadamu kwa mfano Wake Mwenyewe. Hata hivyo, kwa kuwa mwanadamu wa kwanza, Adamu, alitenda dhambi mbele za Mungu(God), watu wote imewapasa kufa mara moja. “Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu” (Waebrania 9:27).
    Kifo cha miili yetu ndiyo njia ya kupita kwenda kwenye uzima wa milele. Wale wasio na dhambi wataingia katika ulimwengu wa milele wa mbingu na kufurahia milele furaha ya kuwa mtoto wa Mungu(God), ilhali wenye dhambi watatupwa katika “ziwa la moto na kiberiti” (Ufunuo 20:10) na watateswa mchana na usiku milele na milele.

    https://www.bjnewlife.org/
    https://youtube.com/@TheNewLifeMission
    https://www.facebook.com/shin.john.35

    Más Menos
    16 m
  • 1. Lazima Kwanza Tujue Dhambi Zetu ili Tukombolewe (Marko 7:8-9, Marko 7:20-23)
    Oct 6 2025

    Kwanza, ningependa kufafanua dhambi ni nini. Kuna dhambi zilizofafanuliwa na Mungu(God), na kuna dhambi zilizofafanuliwa na wanadamu. Neno dhambi, kwa Kigiriki, lina maana ya ‘kukosa shabaha.’ Linamaanisha kutopata sawa. Ni dhambi tusipoyafuata amri za Mungu(God) kwa usahihi. Hebu kwanza tuangalie dhambi kama zilivyofafanuliwa na wanadamu.

    https://www.bjnewlife.org/
    https://youtube.com/@TheNewLifeMission
    https://www.facebook.com/shin.john.35

    Más Menos
    30 m
  • 2. Binadamu huzaliwa wakiwa wenye dhambi (Marko 7:20-23)
    Oct 6 2025

    Kabla sijaendelea, ningependa kukuuliza swali. Unajifikiriaje wewe mwenyewe? Je, unadhani wewe ni mzuri kiasi au mbaya kiasi? Unafikiri nini?
    Watu wote wanaishi chini ya udanganyifu wao wenyewe. Huenda wewe si mbaya sana kama unavyofikiri, wala si mzuri sana kama unavyofikiri.
    Basi, unadhani ni nani ataishi maisha bora ya imani? Je, ni wale wanaojiona kuwa wazuri, au wale wanaojiona kuwa wabaya?
    Ni wale wa pili. Kwa hiyo, ni nani aliye na uwezekano mkubwa zaidi wa kukombolewa: waliotenda dhambi nyingi au waliotenda dhambi chache tu? Wenye dhambi nyingi wana uwezekano mkubwa zaidi wa kukombolewa, kwa sababu wanajijua kuwa wenye dhambi. Wanaweza kukubali vyema zaidi ukombozi ambao Yesu aliwaandalia.

    https://www.bjnewlife.org/
    https://youtube.com/@TheNewLifeMission
    https://www.facebook.com/shin.john.35

    Más Menos
    21 m
Todavía no hay opiniones