Episodios

  • S1E22 Unatumia Siku 28 kwenye Social Media kwa Mwaka: Ijue Gharama Halisi | LENZI | Michael Kamukulu
    Nov 4 2023

    Ijue gharama halishi ya muda ambao unautumia kwenye social media (mitandao ya kijamii). Kwa wastani mtumiaji wa kawaida wa internet anatumia saa 2.5 mpaka 3 kwenye mitandao ya kijamii kwa siku. Mtanzania wa kawaida anatumia wastani wa saa 2.5 kwa siku ambayo ni sawa na siku 28 za kazi kwenye social media kwa mwaka. Huu ni muda mwingi ambao usipotumika vizuri unasababisha hasara kifedha na kiafya pia. Jifunze na upate siri na maarifa zaidi kuhusu ukweli juu ya matumizi ya simu, internet na mitandao ya kijamii. Ungana na Michael Kamukulu kupitia LENZI  @lenzipodcast 

    Más Menos
    4 m
  • S1E21 Digital Detox: Jinsi nilivyojiondoa kwenye addiction ya SIMU na Mitandao | Michael Kamukulu LENZI
    Oct 28 2023

    DIGITAL DETOX Watumiaji wengi hawazifahamu athari zinazotokana na matumizi makubwa ya mitandao ya kijamii, simu, TV pamoja na aina nyingine ya vifaa vinavyotumia screen. Athari hizi zina madhara makubwa sana ikiwemno kusababisha changamoto za afya ya akili. Athari nyingine ni kama matumizi mabaya ya muda, kupunguza ufanisi kwenye uzalishaji, kuvunjika kwa mahusiano pamoja na madhara mengine mengi. Mawasiliano ni kitu cha kuhimu lakini ni muhimu kufuatilia miendendo ya matumizi ya simu za mkononi na mitandao ili kuepuka madhara na athari mbaya. Punguza matumizi makubwa ya mitandao ya kijamii na simu za mkononi ili ulinde maisha na afya yako. Kabla ya kukabiliana na athari hizi, ni muhimu sana mtu akafahamu kama tayari anapitia changamoto hizi au la. Kuna njia nyingi za kutammbua kama umeathiriwa na matumizi makubwa ya simu za mkononi na mitandao ya kijamii. Njia rahisi ni kuangalia kama una mojawapo ya dalili zifuatazo: 1. Kutopendelea kuzungumza na watu, na badala yake kukaa na simu za mkononi au mitandao ya kijamii 2. Kuwa na hali ya wasiswasi uliopitiliza mara kwa mara (Anxiety) 3. Kukosa usingizi (kushindwa kulala vizuri) 4. Kushindwa kutuliza akili (failure to focus) Zipo njia nyingi za kuondokana na madhara ya matumizi yaliyopitiliza ya mitandao ya kijamii na simu za mkononi pamoja na TV.; kati ya hizi ni hizi hapa tano (5): 1. KUTENGA MUDA wa kukaa bila simu/mitandao 2. Kudhibiti APPS 3. Kudhibiti MUDA wa matumizi 4. Kudhibiti MAENEO ya matumizi 5. Balance: Maisha BINAFSI na Maisha ya KAZI Ungana na Michael Kamukulu uweze kujifunza zaidi kupitia LENZI  @lenzipodcast  Chapters 00:00 Madhara: matumizi yaliyopitiliza ya simu na mitandao 01:33 Digital Detox 02:36 1. KUTENGA MUDA wa kukaa bila simu/mitandao 04:26 2. Kudhibiti APPS 06:43 3. Kudhibiti MUDA wa matumizi 08:13 4. Kudhibiti MAENEO ya matumizi 08:39 5. Balance: Maisha BINAFSI na Maisha ya KAZI Jifunze zaidi na Michael Kamukulu kupitia LENZI @lenzipodcast

    Más Menos
    11 m
  • S1E20 Matumizi ya SIMU: Fahamu athari za matumizi yaliyopitiliza ya simu | LENZI | Michael Kamukulu
    Oct 21 2023

    Watumiaji wengi hawazifahamu athari zinazotokana na matumizi makubwa ya mitandao ya kijamii, simu, TV pamoja na aina nyingine ya vifaa vinavyotumia screen. Athari hizi zina madhara makubwa sana ikiwemno kusababisha changamoto za afya ya akili. Athari nyingine ni kama matumizi mabaya ya muda, kupunguza ufanisi kwenye uzalishaji, kuvunjika kwa mahusiano pamoja na madhara mengine mengi. Mawasiliano ni kitu cha kuhimu lakini ni muhimu kufuatilia miendendo ya matumizi ya simu za mkononi na mitandao ili kuepuka madhara na athari mbaya. Punguza matumizi makubwa ya mitandao ya kijamii na simu za mkononi ili ulinde maisha na afya yako. Kabla ya kukabiliana na athari hizi, ni muhimu sana mtu akafahamu kama tayari anapitia changamoto hizi au la. Kuna njia nyingi za kutammbua kama umeathiriwa na matumizi makubwa ya simu za mkononi na mitandao ya kijamii. Njia rahisi ni kuangalia kama una mojawapo ya dalili zifuatazo: 1. Kutopendelea kuzungumza na watu, na badala yake kukaa na simu za mkononi au mitandao ya kijamii 2. Kuwa na hali ya wasiswasi uliopitiliza mara kwa mara (Anxiety) 3. Kukosa usingizi (kushindwa kulala vizuri) 4. Kushindwa kutuliza akili (failure to focus) Zipo njia nyingi za kuondokana na madhara ya matumizi yaliyopitiliza ya mitandao ya kijamii na simu za mkononi pamoja na TV. Fuatilia zaidi uweze kujifunza na Michael Kamukulu kupitia LENZI  @lenzipodcast #mitandaoyakijamii #digitaldetox #mitandao #socialmedia #overused #lenzi #afyayaakili #afyayako #simuyako * * * Timestamps 00:00 Ukweli kuhusu matumizi ya simu na mitandao 01:55 1. Kupendelea kutozungumza na watu 03:49 2. Wasiswasi uliozidi (Anxiety) 04:59 3. Kukosa Usingizi (kushindwa kulala) 05:32 4. Kushindwa kutuliza akili (failure to focus) 06:54 Jinsi ya kujiondoa kwenye madhara ya matumizi makubwa ya simu na mitandao ya kijamii

    Más Menos
    8 m
  • S1E19 Mjasiriamali: YAJUE MAENEO MANNE (4) YA UWEKEZAJI USIOKUWA WA KIBIASHARA | LENZI | Michael Kamukulu
    Oct 14 2023

    Mafanikio hayatokei kwa bahati, wanaofanikiwa wote wanajuia na kuifuata misingi inayowapelekea mafanikio kwa kuwekeza kwenye maeneo yanayoongeza thamani yao kwenye maisha. Siri ya mjasiriamala au mfanyakazi mwenye mafanikio iko kwenye uwezo wake wa kuongeza thamani yake katika biashara au kazi anayoifanya. Thamani huongezeka kwa kuzingatia misingi mkuu ya fedha, maisha na mafanikio. Unaweza kutumia nguvu na muda mwingi kwenye kuikuza biashara na kutafuta mafanikio, lakini mara baada ya kuyafikia mafanikio hayo, ukashindwa kuyafurahji. Unahitaji kufuata misingi ya uwekezaji kwa kuwekeza kwenye maeneo muhimu yatakayokuongezea thamani na kukuwezesha kudumu kwa muda mrefu katika mafanikio yako. Acha mazoea ya kuwekeza kwenye pesa, ongeza thamani maana pesa hufuata thamani. Haya ni maeneo manne (4) yanayofaa kwa uwekezaji usiokuwa wa kibiashara: 1) Afya Imara 2) Elimu & Maarifa 3) Mahusiano bora (ya aina zote) 4) Taaluma (Career) Jifunze zaidi na Michael Kamukulu kupitia LENZI  @lenzipodcast  #mafanikio #biashara #thamani #hela #tanzanianyoutuber #tanzania #kenya #rwanda #timizamalengoyako #lenzi #michaelkamukulu * * * Time Stamps 00:00 Uwekezaji wenye tija 00:32 1. Uwekezaji kwenye Afya 01:59 2. Uwekezaji kwenye Elimu & Maarifa 03:06 3. Uwekezaji kwenye Mahusiano 03:54 4. Uwekezaji kwenye Taaluma (career) 04:48 Fedha inatafuta thamani (money follows value)

    Más Menos
    6 m
  • S1E18 MTUMIAJI WA SIMU: Fahamu njia tano (5) za kuongeza usalama wako mtandaoni | LENZI | Michael Kamukulu
    Oct 7 2023

    Katika zama hizi za kidijitali tulizonazo, kulinda usalama wa taarifa zako kwenye mitandao ni muhimu kuliko ilivyokuwa hapo awali. Jiunge nasi katika video hii tunapoongelea njia tano (5) muhimu za kuimarisha usalama wako mtandaoni. Jifunze jinsi ya kulinda namba yako ya simu, kuweka kinga imara kwenye akaunti zako za baruapepe, kuhifadhi alama za vidole vyako, kujilinda dhidi ya tishio la "deepfake," na kuweka sauti yako salama kutokana na matumizi mabaya kwa njia ya uigizaji wa AI. Epuka vitisho vya kimtandao na kufurahia mtandao usalama zaidi Usisahau kubofya kitufe cha like, kusajili, na kugonga kengele ya taarifa ili kupata taarifa nyingine kama hizi na kuongeza mbinu za usalama wa mtandao! #UsalamaMtandaoni #UsalamaWaMtandaoni #KulindaData #KulindaFaragha #UsalamaWaInterneti #UhamasishajiWaMtandao #UsalamaWaTeknolojia Ungana na Michael Kamukulu ili ujifunze zaidi kupitia LENZI  @lenzipodcast  #mpesa #usalama #cybercrime #cybersecurity #email #iphone #iphone15 #mafanikio #biashara #thamani #hela #tanzanianyoutuber #tanzania #kenya #rwanda #timizamalengoyako #lenzi * * * Time Stamps: 00:00 Uhalisia kuhusu usalama mtandaoni 01:04 1. Namba ya Simu 01:37 2. Email / Baruapepe 02:50 3. Fingerprint / Alama za vidole 03:35 4. Sura 04:50 5. Sauti

    Más Menos
    7 m
  • S1E17 Jinsi ya Kufanya Manunuzi Salama Mtandaoni: Mambo Matano (5) ya Muhimu | LENZI | Michael Kamukulu
    Sep 30 2023

    Watu walio wengi hawajui jinsi ya kununua bidhaa kwa njia salama kwenye mtandao kama vile Alibaba, Amazon, Kikuu, Ali Express na mitandao mingine ya aina hii. Kabla ya kuagiza bidhaa kwenye mtandao au simu, ni muhimu kuhakikisha kwamba pesa yako iko salama na unanunua kwa wauzaji wanaoaminika. Unaweza kutumia njia kama vile M Pesa, Tigo Pesa, Airtel Money au nyingine kama vile Sim Banking. Na unaweza pia ukaagiza buidhaa kwa delivery na ukalipia cash baada ya kupokea bidhaa yako. Ni muhimu kujua Mamboi matano (5) muhimu ambayo yatakusaidia kuwa salama wakati wa manunuzi ya mtandaoni: 1. Kuwa na Akaunti Maalum ya Malipo 2. Nunua kwa Wauzaji Wanaoaminika 3. Tunza/Ficha Taarifa Zako zote Muhimu 4. Fanya Mawasiliano ya kina na Muuzaji kabla ya kununua/kulipia 5. Usifanye Manunuzi Makubwa kwa njia ya Mtandao Fuatilia na ujifunze zaidi na Michael Kamukulu kupitia LENZI  @lenzipodcast 

    Más Menos
    5 m
  • S1E16 Harufu Ya Chakula Haitibu Njaa: Furaha inayotegemea kuwaridhisha watu wengine bila faida binafsi, ni UTUMWA
    Sep 23 2023

    Njaa hutibiwa na chakula, wala harufu nzuri na hata sio lazima chakula kiwe kitamu sana. Haijalishi kama kinaliwa jioni, mchana, asubuhi wala usiku. Harufu ni hisia inayokuvutia kuelekea kwenye chakula, lakini usipokula hicho chakula, njaa haitaondoka. Hii inatokea sana kwenye maisha yetu ya kila siku katika kutafuta mafanikio ya career, mahusiano, nk. Tunahitaji maarifa sahihi ili kufanya maamuzi sahihi yatakayotupa kufanikiwa kwenye kazi, kukuza faida kwenye biashara, kuongeza wigo kama viongozi / kiongozi, kuboresha mahusiano ndani na nje ya ndoa pamoja na mambo mengine mengi. Mojawapo ya njia za kuongeza mafanikio yanayotokana na maamuzi yetu ni kujitambua, kuweka malengo na kuwa na uwezo wa kuyapima malengo kwa kipimo sahihi. Zipo siri na kanuni nyingi ambazo zinaweza kumsaidia kila mtu, lakini walio wengi wamechagua hisia kuliko uhalisia. Watu wengi hupima mafanikio ya maamuzi yao katika maisha, biashara, mahusiano hata kazi kwa kuangalia ni kwa kiasi jamii ikiyowazunguka inaridhishwa. Hata kama itahusisha maumivu, hasara au majuto, bado watu walio wengi wako tayari kufanya jambo wasilolitaka ilimradi wengine wawakubali na kuwaheshimu. Si mara zote matokeo yanakuwa chanya, na ndio maana kuna umuhimu wa kuangalia faida zote, binafsi na zile za jumla ili matokeo ya maamuzi yoyote yale yasije yakaishia kuwa majuto, hasira, chuki, aibu ama kukata tamaa. * * * Hadithi/Simulizi Mtoto (yatima) aliomba chakula cha kwake na wadogo zake ili wasife njaa baada ya kukaa siku nyingi bila mlo wowote. Mtu mzima aliyeombwa chakula alimjibu kwa kutoa ushauri, “chukua kitunguu swaumu ukakichome kwenye moto, majirani wakisikia watasema mmepika na kuka chakula kizuri”. Huu ushauri haukulenga kutatua tatizo halisia, ulilenga kuionesha jamii kwamba hakuna tatizo wakati huo huo madhara yakiendelea kutokea kwa watoto. * * * Ongeza uwezo wako katika kufanya maamuzi sahihi kwa kutumia njia bora ambazo hazina madhara. Sikiliza uweze kujifunza zaidi na Michael Kamukulu kupitia LENZI |  @lenzipodcast 

    Más Menos
    3 m
  • S1E15 Ishara 5 kwamba unapoteza kuliko unavyopata (unapoteza MUDA, THAMANI, FEDHA kwenye kazi na biashara)
    Sep 16 2023

    Kama hasara ama gharama ya kupata jambo lolote inakuwa kubwa kuliko faida zinazotokana na jambo hilo, basi hatuna budi kuachana na jambo husika na kutafuta mbadala unataofaa na kutupa manufaa tunayoyahitaji. Kama gharama za matumizi zinazidi kiwango cha mshahara ama faida ya biashara, ni wakati wa kubadilisha kazi au biashara hiyo. Mara nyingine inakuwa vigumu kufahamu kwamba tayari uko kwenye hali ya kupoteza na kuliko kunufaika. Hizi ni ishara 5 kati ya nyingi zinazokufungua macho ili kujua kwamba ni wakati wa kufanya jambo tofauti. 1. Gharama za matumizi ni kubwa kuliko kipato (mshaharara au faida ya biashara) 2. Kutokuona mabadiliko (matokeo) yanayotokana na kazi au biashara 3. Kushindwa kumiliki na kusimamia muda na ratiba binafsi 4. Kushindwa kuishi katika uhalisia wa ndani (failure to be your authentic self) 5. Kushindwa kutumia uwezo binafsi (vipaji na karama) Ungana na Michael Kamukulu ili kujifunza zaidi kupitia LENZI |  @lenzipodcast 

    Más Menos
    9 m